Contact Info

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Kufuatia juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) na Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) katika kutatua mgogoro uliokuwepo UMATI, napenda kuutarifu umma kuwa wanachama hai na wenye mapenzi mema na Shirika la Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) walifanikiwa kupitia na kuidhinisha Katiba na Kanuni za Shirika zinazozingatia Sheria na miongozo ya uendeshaji wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Mchakato huu uliwezesha kufanyika mikutano kadhaa ukiwemo wa uchaguzi wa viongozi wa wanachama kwa kuzingatia katiba na kanuni za shirika la UMATI pamoja na sheria na miongozo ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Kwasasa Shirika la UMATI lina uongozi halali kwa mujibu wa katiba ambao ni Mwenyekiti, Katibu, na Mweka Hazina.
Aidha, ninapenda kutoa taarifa kuwa uongozi uliopo uliitisha Mkutano Mkuu tarehe 9 Januari 2026, ambapo pamoja mambo mengine, ulichagua wajumbe 7 wa Bodi ya Wagurugenzi wa Shirika kwa kuzingatia Sheria na Miongozo ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwa kuzingatia viwango vya utawala bora vya International Planned Parenthood Federation (IPPF). Wajumbe hao walichaguliwa kwa kuzingatia uzoefu wao wa kitaaluma na utaalamu katika maeneo ya sheria, ukaguzi wa hesabu ya fedha, mawasiliano, afya, utawala bora, na uhamasishaji wa rasilimali.

Bodi ya Wakurugenzi imefanikiwa kupatiwa mafunzo ya awali (induction) ambayo yalifanyika tarehe 20 na 21 Januari 2026 kwa kushirikiana na wakufunzi kutoka IPPF.

Aidha, Uongozi wa UMATI unapenda kuutaarifu umma kwamba kumekuwepo na taarifa za upotoshwaji na tuhuma mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii zilizolenga kulichafua Shirika letu, Ofisi ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na NaCoNGO kuwa Shirika linajihusisha na miradi isiyofuata maadali na tamaduni za nchi. Kwa taarifa hii, napenda kutoa taarifa kuwa, habari hizo hazina ukweli wowote na kwamba shirika limetoa taarifa kwa vyombo husika na zinafanyiwa kazi ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.

Mwisho, napenda kuwataarifu kuwa, kwasasa UMATI ina jumla ya wanachama hai wapatao 51 ambayo orodha yao imeambatinishwa na taarifa hii. Napenda kumshukuru Muheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na Uongozi wa NaCoNGO kwa juhudi kubwa walioifanya kuhakikisha UMATI inasimama imara na kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuchangia juhudi za serikali na kuwafikisha hutuma Watanzania.

Pia, natoa shukrani za dhati kwa wanachama hai wa UMATI kwa juhudi zao katika kuhakikisha Shirika hili linaendele kuimarika na kuendelea majukumu yake.
Wenu katika Ujenzi wa Taifa.

Majina ya Wanachama Hai

S/N Name
1 David  M Lucas
2 Abdallah Jafari Chaurembo
3 John  Maliyapamba  Komba
4 Agatha Peter Haule
5 Benedicta  Josephine Sinzo Maganga
6 Thabit Badi Lema
7 Husna Boniface  Wangwe
8 Esteria Joachim Kisoka
9 Latifu Abdulrahmani Saidi
10 Sosthenes  Stephen Amasi
11 Laurencia  Enock Ndali
12 Kassimu Omari Abdallah
13 Alice Robert Mwantobe
14 Magdalena Honest Kawishe
15 Gertrude Nicodem Naphtali
16 Angel Lucas Pinda
17 Grace Christopher Masawe
18 Jamali Juma Kimbo
19 Pius John Isaack
20 Rehema Athuman Nkungu
21 Gerald Vitus Kihwele
22 Kabora Elisha Kabora
23 Fredinandy Sylvester Nyamonge
24 Issaya Jacobo Laizer
25 Yahaya Kwatta Hussein
26 Herry Eliufoo Christopher
27 Fidelis John Owenya
28 Priscus Tarimo
29 Maiko Joseph Ernest
30 Mpeligwa Gwakisa Emmanuel
31 Hafidhi Yahaya Lumbi
32 David Joseph Mwamwaja
33 Linda Raphael Kyando
34 Prince Gwamaka Mwaihojo
35 Edmund E. Mwandebwa
36 Richard A. Kajala
37 Saidi Mussa Nyengedi
38 Charles Mashilanga Mashilanga
39 Charles NtwaleLlukas
40 Mufandii Hamisi Msaghaa
41 Norbert Faustus Masebe
42 Bernard Emmanuel Yombayomba
43 Anastazia Kifuku
44 Bibiana Afred Kasochela
45 Charles Simon Yakusola
46 Moses Bonifas Kandege
47 Daniel David Mtamakaya
48 Zenna Hussen haji
49 Cuthbert David Maendaenda
50 Mohamed Mustapha
51 Julius Samweli Madiga

Kwa maelezo zaidi Pakua Barua rasmi ya Taarifa hii: Hapa